- Mbunge huyo alimposa Naiya Ntuntu katika sherehe za kusherehekea siku ya kuzaliwa baada ya miaka miwili ya uhusiano
- Ngeno amekuwa akisukumwa sana na jamii yake na marafiki wakiwemo wanasiasa hadi akatii amri, akakubali kumposa mpenziwe
Aliyekuwa anatambulikana kama baba wa makapera katika chama cha KANU hatimaye ameyakomesha maneno ya wapinzani na marafiki zake waliokuwa wakihoji kuwa hana mke wala mpenzi.
Habari Nyingine: Raila Junior ashambulia wanaomtaka babake kuzungumzia ufisadi nchini
Johanna Ngeno, mbunge wa eneo bunge la Emurua Dikirr alifichua kupitia kwa ukurasa wake wa Facebook kuwa alishajipatia mpenzi na hata kumposa katika hafla moja ya kusherehekea siku ya kuzaliwa.

Habari Nyingine: Kipusa Mkorino asisimua mitandao kwa picha maridadi, ni mrembo ajabu
Hii ni baada ya kumposa mpenziwe wa miaka miwili, Naiya Ntutu, ambaye ni wakili maarufu jijini Nairobi kutoka kaunti hiyo ya Narok siku ya Ijumaa, Juni 1.
Ndoa hiyo ya kitamaduni ilihudhuriwa na Waziri Charles Keter, Charles Korir, Farouk Kibet, Alfred Keter, Oscar Sudi, Wilson Sossion, Sabina Chege na Gabriel Tongoyo.

Habari Nyingine: Barua ya mapenzi ya mwanafunzi wa shule ya upili kwa mwalimu wake yasisimua wengi

Mbunge huyo alikuwa amedai hapo awali kuwa kamwe hatofunga pingu za maisha hadi pale atakapoaga siasa.
Read ENGLISH VERSION
Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibIJ3fpdmpJutnpyybrfAraCkmV2grq6uyGawmmWblru2ecCmp6irkWK6sbHNs6CwnV2srm65yJqimmWblrGprY2hq6ak